Posts

JUMLA YA MALALAMIKO 78 YA RUSHWA YARIPOTIWA MKOANI KATAVI.

Image
Jumla ya malalamiko 78 ya vitendo vya rushwa Mkoani Katavi yameripotiwa katika taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa katika kipindi cha mwezi Julai 2017 hadi Machi 2018. Akitoa taarifa ya mwaka kwa Vyombo vya Habari Kaimu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi Ndugu Christopher Lawrence Nakua amesema,taarifa zilizopokelewa zimeainisha Idara na Taasisi mbalimbali zilizotuhumiwa na vitendo vya Rushwa ikiwa ni Taasisi za serikali na Binafsi. Ambapo Halmashauri Kimkoa zina jumla ya malalamiko 78,Polisi malalamiko 6,Chama cha Ushirika malalamiko 2,Idara ya Afya malalamiko 6,Sekta binafsi (BAYPOT na PRIDE) malalamiko 2. Mashirika ya Umma (TANESCO na TARULA) malalamiko 3,Idara ya Elimu malalamiko 5,Idara ya Mifugo malalamiko 2,Idara ya Uvuvi lalamiko 1 na Ofisi ya Makazi ya Wakimbizi lalamiko 1. Aidha,Idara na Taasisi zingine zilizotajwa ni pamoja na uhamiaji lalamiko 1,Idara ya Ardhi malalamiko 5,Idara ya Ujenzi malalamiko 3,Serikali ya Vijiji malalamiko 10 na Sekta ya Madini lala...

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya Februaly 19 2017.

Image
Magazeti ya Februaly 19 2017 kuhusu post zote kubwa zilizobebwa kwenye Magazeti ya Tanzania kuanzia kwenye, Udaku ,  Hardnews  na  Michezo  ili uje kinachoendelea.

MAMA MMOJA MKOANI MBEYA AMEFUKUA KABURI LA MWANAE KWA KILE ANACHODAI ANGEFUFUKA BAADA YA SIKU YA 3

Image
Katika hali ya kushangaza Mama mmoja anayefahamika kwa jina la Lusi Shegeleti (52) mkazi wa Mbalizi Mkoani Mbeya amefukua kabri la mwanaye baada ya wananchi kuuzika mwili wa mtoto huyo kwa kile anachoamini mwanae bado hajapoteza maisha. Akizungumza na Sweet Fm Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishina wa Polisi Dhahiri Kidavashari ameasema, Mtoto huyo Baraka Mwasengo amefariki tarehe 15 mwezi huu na kuzikwa tarehe 16 ambapo usiku wa kuamkimkia leo mama huyo alichukua vi jana wawili na kwenda kulifukua kaburi kisha kuurudisha mwili wa mtoto huyo ndani kwaajili ya maombezi kwa kile anachodai mwanae angefufuka baada ya siku tatu.  Aidha,baada ya wananchi kutoa taarifa kituo cha Polisi, Jeshi la Polisi limefika nyumbani kwa mama huyo na amekiri kuufukua mwili huo na kaburi limekutwa jeneza tupu ambapo mwili wa mtoto huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Ifisi na mama huyo anashikiliwa na Jeshi kwaajili ya taratibu za kisheria.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili ya January 15 2017.

Image
Magazeti ya January 15 2016 kuhusu post zote kubwa zilizobebwa kwenye Magazeti ya Tanzania kuanzia kwenye, Udaku ,  Hardnews  na  Michezo  ili uje kinachoendelea.